Nibaada ya diplomasia ndefu anayoendelea kutekeleza kwa ajili ya amani na usalama katika kanda nzima ya maziwa makuu africa ya kati,Africa Kusini na Africa mashariki , Waziri Mbusa Nyamwisi, amefaNikiwa kumrejesha katika siasa Marie-Madeleine Kalala ambae kwa sasa ameingia katika Kamati ya Wazee wa CEEAC.
Hii ni badaa Ushawishi Mkubwa wake Mbusa Nyamwishi ambae amefanya ziara hapa na pale katika lengo la kujenga ushirikiano mpya kati ya Congo na majirani zake pamoja na kuimarisha umoja kati ya wananchi wa Congo DRC kwa ajili ya amani,usalama na maendeleo.
Madeleine Kalala alikuwa Waziri wa Haki za Kibinadamu, katika serikali zilizo pita na kwa sasa ameteuliwa kushiriki katika Kamati ya Watu Wenye Hekima ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (CEEAC), Hii imefanyika Mjini Kinshasa Jumatatu hii Julai 24, 2023 na kuishukuru Serikali yake Felix Tshisekedi kwa heshima amepewa na kusukuma gurudumu la wanawake mbele zaidi .
Bi Kalala amepongeza Wizara ya Ushirikiano wa Kikanda kwa kazi kubwa wanazo zifanya kwa ajili ya kuimarisha kwa maranyingine shura Mpya kwa DRC ambayo hivi karibuni itajikwamua katika matatizo mbali mbali kupitia Diplomasia.
Mbali na kuteuliwa katika Kamati ya Wazee ya CEEAC, Marie Madeleine Kalala ameteuliwa kuwa mkuu wa ujumbe wa ukaguzi kura ya maoni katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bi Kalala anasema anajivunia kuwakilisha nchi yake na anaahidi kufanya kazi bora kwa heshima ya wanawake barani Afrika.
Kalala alikuwa mwanaharakati wa haki za wanawake wa Kongo.Alikuwa Waziri wa Haki za Binadamu wa DRC kuanzia mwaka 2003 hadi 2007, mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mjumbe wa jopo la watu wenye hekima wa Umoja wa Afrika.