Abdou Masirika, ni jina la Kiongozi mmoja wa magaidi wa ADF aliye uliwa jumapili JULAI 9, na wanajeshi wa operesheni ya pamoja kati ya Congo na Uganda, FARDC-UPDF. Gaidi huyu aliuwawa karibu na mto Talia katika sekta ya Ruwenzori mkoani Beni Kivu kaskazibi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemocratia ya Congo.
Msemaji wa operesheni ndiye apatoa habari ya ku uwawa kwa gaidi huyo.
"Abdou Masirika ni mzaliwa wa Tanzania. Huyu anashirikiana na gaidi mwengine Sheikh Chamalanda, aliye endesha mashambulizi kadhaa katika eneo la Kabasha-Maboya kwenye barabara la taifa nambari mbili. Vikosi vya FARDC-UPDF vilimkuta aki zagaa zagaa maeneo ya mto Talia nani hapo ndipo aliuliwa", aeleza Luteni kanali Mak Hazukay.
Jeshi la Congo na la Uganda, zaendesha operesheni ya pamoja kwa lengo lakukata mlolongo wa usambazaji wa ADF/MTM.
Ni pamoja na operesheni hizo ndio ilipelekeya kuangamiza wagaidi wengine watatu wa ADF/MTM katika bonde la Mughalika mkoani Beni usiku wa JULAI 9.
Eneo la Beni la kabiliwa na mashambulizi ya magaidi wa ADF/MTM tangu mwaka wa 2014. Ma milioni ya raia wameuwawa kwa mapanga, magari mingi kuunguzwa yaeleza shirika la raia. Aidha ya operesheni ya FARDC-UPDF, Majeshi ya Congo FARDC yaendesha piya operesheni SOKOLA 1 katika maeneo hayo kwa le lengo lakusitawisha usalama kwa kupambana na vikundi vya kijeshi vya nyumbani na magaidi wa ADF/MTM.