Sherehe hizo zilizoanza kwa kutembelea Hospitali ya wilaya ya Chalinze, Msoga ambapo wakiwa Hospitalini hapo, Naibu Waziri Mhe.Kikwete ambaye aliongozana na Wauguzi wa Mkoa wa Pwani walipata nafasi ya kutembelea wodi ya Wazazi ambapo pamoja na shughuli nyenginezo waligawa taulo kwa watoto wachanga, sabuni za kufuria na za kuogea kwa wazazi wote waliojifungua watoto.
Akizungumza na Wauguzi wa mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mhe. Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwaasa Wauguzi kuwa Wazalendo katika utendaji kazi wao huku akiwasisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua changamoto wanazokabiliana nazo na kuwaahidi kuwa serikali inaendelea kuzishughulikia changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwa pamoja na mifumo iliundwa kusaidia utendaji bora Kazini.