Uwepo wa waasi wa Uganda wa ADF kwenye vijiji mbali mbaliko mkoani Ituri hasa wilayani Mambasa wazua wasiwasi zaidi wakazi wa eneo hilo ambalo wamethibitisha kwamba waasi hao wanaonekana zaidi katika eneo la uchifu la Babila Bakwanza, eneo la Mambasa zaidi ya kilomita 160 kusini mwa mji wa Bunia, Mji mkuu wa jimbo la Ituri.
Mashirika ya kiraia ya Kongo ikitahadharisha mamlaka za usalama kutekeleza majukumu yao kikamilifu katika kutokomeza tishio lililopo Mabukulu na Babuludjo, maeneo mawili yaliyoko takriban kilomita ishirini kutoka kituo cha Mambasa kwenye mhimili wa Komanda.
Tayari wakiwa njiani waasi hawa walichoma nyumba tano za wakazi wenye amani kabla ya kuvuka RN 4 eneo ambalo wakulima kadhaa wanalima shamba zao.