Kuanzishwa rasmi kwa Kanda Maalum ya Kiuchumi ya Kin Malebo ni hatua kubwa katika maendeleo hasa katika viwanda vya miti na mbao za Congo DRC; Juma nne Mjini Kinshasa Waziri wa Viwanda, Julien Paluku Kahongya aliwasilisha rasmi amri ya wizara yake inayoidhinisha mkataba wa maendeleo kati ya Wakala wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi-AZES na Kampuni ya Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda vya Kongo- SIDIC/ARISE, kwa Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi za Umma ambazo huingilia kati katika Kwakuwapa faida wawekezaji katika eneo hilo linalo patikana mashariki mwa Mji wa Kinshasa.
Katika hafla hii, Waziri wa Viwanda aliwaomba Wasimamizi Wakuu hawa kuongeza uelewa utawala huu mpya wa kiuchumi uliowekwa na Jimbo la Kongo. Kontena za kwanza zenye sehemu za viwanda na mitambo mbali mbali zikiwa tayari kwenye bandari ya Matadi alisema Romain Deniel, Mkurugenzi Mkuu wa SIDIC. Kwa upande wa DGDA, Mkurugenzi Mkuu , Bernard Kabese alihakikisha kwamba vifaa hivyo vyote vitatolewa ,huku akiongeza kuwa wafanyakazi wake tayari wamepelekwa katika eneo husika eneo la majaribio ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi wa Maluku ambapo uzalishaji wa kwanza wa vigae na udongo utakaotengenezwa nchini Kongo utazinduliwa baada ya wiki chache. Ikumbukwe kwamba Wakurugenzi Wakuu wa Mashirika ya Umma wakiwemo wa AZES, FPI, DGDA, OCC, DGI, DGRAD na OGEFREM wamepokea agizo hili la kati ya wizara.