Waasi wa M23 waombwa kuweka silaha Chini haraka iwezekanavyo nakuji ripoti katika kambi ya kijeshi ya Rumangabo ipatikanayo wilayani Rushuru, Kivu Kaskazini, mashariki mwa Kongo.Hatuwa kutoka kwa viongozi wa Afrika mashariki, akisema Mbusa Nyamwisi, waziri wa ushirikiano wa kikanda wa DRC.
Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda, Mbusa Nyamwisi Antipas aliwasili Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Jumanne hii JULAI 11, 2023 NA Kulakiwa na umati wa watu hasa wafuasi wa Chama Chake cha RDC /KML Nyamwisi masema kuna ujumbe wa kitaifa na wa kikanda unaotarajiwa kuwasili Goma kuhuzuria mkutano Muhimu kuhusu hali ya usalamana na amani Mashariki mwa Congo DRC.
Kwa mujibu wa Mbusa Nyamwisi, ziara hii ni sehemu ya kuimiza wakazi wa mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Akizungumza na vyombo vya habari vya kye uwanja wa ndege wa Goma , Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda alisema, misheni ya safari yake ni sehemu ya mchakato unaoendelea kufatia hatua kadhaa zilizo chukuliwa na viongozi wa serikali mbali mbali za Africa mashariki kwa ajili ya kumaliza uasi wa M23 uasi unao sababisha maelfu ya wakaazi kubaki wakimbizi wa ndani katika taifa lao.
Alipowasili kwenye ndege alitangaza ujio wa makamu waziri mkuu na Waziri wa Ulinzi wa DRC jEAN_ PIERRE Bemba Pamoja na ujio wa Rais wa zamani wa Kenya, UHURU KENYATA, ambaye ndiye msuluhishi wa mgogoro wa mashariki mwa kongo kwa sasa.
Hayo yana jiri wakati ambapo kuna ujumbe kutoka bunge la Afrika mashariki, ambao umewasili Goma tangu jumatatu hii, wakiwa na lengo la kukutana na makundi mbali mbali yakiraia, pamoja na viongozi wa serikali wa mkoa wa kivu kaskazini.
Waasi wa M23 wakitangaza kuwa swala la kusalimisha silaha hali wahusu, kabla hakuna kuweko mazungumzo ya moja kwa moja kati yao na serekali ya Kinshasa.
Utafahamu kwamba, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo imeandikisha idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na Waasi wa M23 wilayani Rushuru, Masisi na sehemu moja ya Nyiragongo, kivu Kaskazini.