Rais wa jamhuri yakidemokrasia ya congo, Félix Tshisekedi, ameunda upya jeshi la congo (FARDC).
Ni kupitia maagizo kadhaa yaliyosomwa kwenye televisheni ya taifa (RTNC) usiku wa Alhamisi Desemba 19, 2024 ambapo rais wa Nchi alichukua maamuzi makubwa ya kujaribu kurekebisha hali hiyo wakati nchi inapitia mgogoro na mvutano inayohusishwa na ugaidi wa wapiganaji wa Allied Democratic Forces (ADF) katika sehemu ya mashariki na kaskazini mashariki mwa majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.
Wakati wa kusomwa, ilibainika kuwa Jenerali wa Jeshi Christian Tshiwewe, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alibadilishwa na Meja Jenerali Jules Banza Milambwe . Jenerali Tshiwewe Christian, ambaye alibadilishwa, hata hivyo aliteuliwa kuwa mshauri wa kijeshi wa rais.
Meja Jenerali Tshitambwe Chiko ambaye hadi sasa alikuwa kamanda wa Operesheni za Kaskazini dhidi ya Vuguvugu la M23 na naibu mkuu wa jeshi anayesimamia operesheni na ujasusi aliteuliwa kuwa kamanda wa kanda ya kwanza ya ulinzi.
DESEMBA 20, 2024
| Germaine Hassan Kyahwere
Kando na haya, endelea kuskiliza matangazo zaidi kutoka MTV
Radio