Leo ikiwa siku ya kimataifa ya mama wa Africa wanawake wanao patikana katika kambi mbali mbali mashariki mwa Congo DRC waomba makundi ya waasi na serikali kuwasikilia huruma wanawake na watoto wanao endelea kuteseka kila siku kutokana na vita visivyo na lengo kwa maendeleo ya Bara la Africa hasa akina mama wakionekana kuwa waathirika wa Kwanza.
Kwa sasa DRC inaripoti idadi kubwa ya wakimbizi hasa eneo lake la mashariki ambako kuna uasi wa M23 Kivu kaskazini, Rutshuru ,masisi na nyiragongo na eneo la Beni na sehemu moja ya Ituri kukiripotiwa kundi la kigaidi la ADF .wanao umia sana ikiwa ni wanawake na watoto kuuwawa,kubakwa na kuzalilishwa .wanawake wameoma wapewa amani na usalama wa kudumu kuanzia sasa kwani hakuna uzima bila mwanamke.