Waziri Mkuu wa Kongo ya Kidemkrasia na mwenziye wa Kongo Brazaville wakutana kumaliza tofauti bahina ya mataifa yao.
Mkutano wao uliofanyika Pembezoni wa michezo ya Olimpiki , inayo shirikisha mataifa zinazo tumia kifaransa kama lugha rasmi Duniani jijini Kinshasa Mji mkuu wa Kongo ya Kidemkrasia . Waziri Mkuu wa DRC Bw. Sama Lukonde na mwenziye wa Kongo Brazaville Bw. Makosso Anatole walikutana kwa mazungumzo , katika kile kinacho elezwa kama kuchunguza mwenendo wa hali ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo jirani katika kanda ya Afrika ya kati.
Kupitia akaunti yake ya twitter , waziri wa habari na msemaji wa serikali ya DRC Bw. Patric Muyaya , ame fafanua kwamba mawaziri hao wali papasia pia namna gani , kusukuma mbele miradi zao za pamoja kati ya Kinshasa na Brazaville.