DRC

Zoezi la uboreshaaji daftari la wapiga kura kuanza julai20, 2024

JUNI 24, 2024
Border
news image

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi Maalum la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura  na kuanza rasmi Juni 20 hadi 26, 2024 badala ya Juni 1, 2024 mkoani hapa.

Akitoa Taarifa kupitia vyombo vya Habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa Jackobs Mwambegele amesema tume imezingatia maoni na ushauri kutoka kwa wadau katika kuratibu mchakato mzima wa zoezi hilo na kuamua kulisogeza mbele.

Jaji Mwambegele amewataja wadau waliokutana na tume na kutoa maoni na ushauri  kuhusu utekelezaji wa zoezi hilo kuwa ni viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa dini, wawakilishi wa Asasi za kiraia, Wahariri wa vyombo vya Habari, waandishi wa Habari, Maafisa Habari, wawakilishi makundi ya vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na wazee wa kimila.

Amesema  wadau hao wameomba kusogezwa kwa zoezi hilo ili kuipa nafasi Tume kutoa Elimu kwa Mpiga kura, Taasisi angalizi kupata fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wakati wa utekelezaji wa zoezi sambamba na vyama vya siasa kutafuta mawakala na kuhamasisha wafuasi kushiriki katika zoezi hilo.

AM/MTV News DRC