TANZANIA

ZIARA YA MAKONDA YAAHIRIDHWA KUOMBOLEZA KIFO CHA LOWASSA

FEBRUARI 11, 2024
Border
news image

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM paul Makonda amelazimika kukatisha ziara yake ya kusikiliza kero kwa wananchi wa mikoa ya 2 Lindi na Mtwara ili kuwapa wananchi fursa yakuomboleza kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mhe.Edward Lowassa kilichotokea siku ya jana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI siku ya tarehe 10.02.2024 Jijini Dar es salaam.

Aakitoa tamko hilo la Chama cha Mapinduzi CCM Mwenezi Makonda amesema mchango uliotolewa na Marehemu Lowassa kwa Taifa ni mkubwa hivyo ni vyem kuwaacha wananchi na chama kwa pamoja kuomboleza na kumuombea kiongozi huyo.

Mbali na hapo Mwenezi Makonda amevishauri vyama vingine vya siasa nchini Tanzania kuungana kwa pamoja na kusitisha shughuli zao kwa kipindi hichi cha maombolezo ya kiongozi wa taifa ili kuwapa nafasi wanachama kuombolea.

MTV Tanzania