TANZANIA

WIZARA YA AFYA TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA TRILIONI 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND

JANUARI 31, 2024
Border
news image

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa kiasi cha Tsh. Trilioni 1.4 kutoka Global FUND ili kutekeleza afua mbalimbali za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria nchini kote kwa malengo endelevu ya Milenia ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifika mwaka 2030.

Upokeaji wa msaada huo umefanyika chini ya Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa pamoja wameshuhudia utiji saini wa makabidhiano ya msaada huo baina ya Global Fund na Serikali ya Tanzania.

“Msaada huu wa fedha unalenga kutekeleza afua mbalimbali za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria nchini kote lengo likiwa ni kutekeleza malengo endelevu ya Milenia ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifika mwaka 2030". Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy amewashukuru Global Fund kwa msaada huo mkubwa katika Sekta ya Afya na kwa kuridhia ombi la Sekta ya Afya kutumia frdha za msaada kutoka Global Fund kwa ajili ya kusomesha na kuwaajili wataalam wa Afya ngazi ya jamii (Community Health Workers) wapatao elfu Tano kwa kipindi cha miaka Mitatu ijayo ambapo wataalam hawa watasaidia kuleta mabadiliko ya utoaji wa huduma za Afya nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Global Fund katika sehemu ya High Impact Africa 2 Bw. Linden Morrison ameipongeza Tanzania kwa kushika nafasi ya Nne Kati ya nchi zinazopokea fedha hizo kutoka Global Fund.

“Lakini pia naipongeza Tanzania kwa kuendelea kutumia vizuri fedha hizo za msaada kutoka GLOBAL FUND ambapo Tanzania imefikia asilimia 92 ya utumiaji wa fedha hizo na hali hii inapelekea kuzifikia afua nyingi katika maeneo ya Kifua Kikuu, UKIMWI nà Malaria”. Amesema Bw. Morrison.

MTV Tanzania