DRC

Waziri Mkuu Wa Tanzania Kassim Majaliwa Aagiza Hifadhi Za Taifa Ziongeze Vivutio Kwa Watalii

MACHI 26, 2025
Border
news image

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Shirika la Hifadhi za Taifa nchini humo kuanzisha programu za kutangaza vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ili kuongeza idadi ya watalii wanaoingia katika hifadhi hiyo.

Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa ikiwemo ujenzi wa barabara, lango la watalii na huduma nyingine za kijamii ndani ya hifadhi hiyo hivyo ni lazima sasa Mamlaka hiyo itumie fursa hiyo kuongeza idadi ya watalii.

Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wahifadhi na wananchi baada ya kuzindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lililoko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa kuweka mkakati wa kuimarisha mawasiliano katika njia na maeneo yaliyoko ndani ya hifadhi hiyo.

Olive Nyeriga TZ