DRC

Waziri Mkuu Wa Tanzania Aagiza Wasio Raia Kutojiandikisha Kwenye Daftari La Kudumu La Mpiga Kura

JULAI 16, 2024
Border
news image

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kasim Majaliwa ameitaka tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kushirikiana na Viongozi mbalimbali, Wananchi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha hakuna raia wa kigeni atakaejiandikisha katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura.

Majaliwa ametoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa daftari za kudumu la mpiga kura lililofanyika kitaifa mkoani kigoma ambapo waziri mkuu amesema daftari hilo linawahusu Watanzania pekee na si raia wa kigeni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegere amesema zoezi hilo limezindiliwa mkoani Kigoma na litaendelea kwa mikoa mitatu ya kigoma tabora na katavi kwa siku saba kuanzi julai 20 hadi julai 27 mwaka huu na badae litaendelea katika mikoa ya Kagera na Geita na mikoa yote nchini.

Awali akitoa mkuu wa mkoa wa kigoma Thobias Andengenye amesema serikali ya mkoa huo imejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa ili kuwezesha wananchi wa mkoa wa kigoma na watanzania kwa ujumla wanapata fursa ya kushiriki uchaguzi mkuu mwakani 2025.

AM/MTV News DRC