TANZANIA

Watumishi Wa Ardhi Mwanza Kufanyiwa Mabadiliko Makubwa

MACHI 16, 2024
Border
news image

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania Mhe. Jerry Silaa ameahidi kufanya mabadiliko makubwa kwa watumishi wa sekta ya ardhi jijini Mwanza kwa kusababisha migogoro inayoleta vilio kwa wananchi.

Waziri Silaa amesema hayo katika viwanja vya Nyamagana ambapo Kliniki ya Ardhi ilikuwa ikifanyika kwa wakazi wa Jiji la Mwanza kuwasilisha kero zao za ardhi na kutatiliwa papo hapo na Waziri Silaa.

Waziri Silaa amesema hayo baada ya kuwepo kwa vilio vingi vya wananchi waliodhulumiwa ardhi zao ambapo chanzo kikuu kikionekana ni watumishi wa sekta hiyo jijini Mwanza.

Aidha, miongoni mwa Mkwakazi hao walio na vilio ni Theopista Alphonce kutoka mtaa wa Nyasaka jijini Mwanza ambaye anaangua kilio mbele ya watu baada ya kuluwezeshwa na Waziri Silaa kupata haki yake iliyokuwa inamsumbua kwa muda mrefu wakidai.

MTV Tanzania