Tanzania

Watumishi Wa Afya Watakiwa Kuenda Kufanya Kazi Maeneo Ya Pembebzone Mwa Nchi

JULAI 29, 2024
Border
news image

Watumishi wa Afya nchini wametakiwa kwenda kufanya kazi katika Halmashauri za pembezoni mwa nchi ili kupunguza uhaba wa wataalamu hao unaokadiriwa kuwa ni zaidi ya asilimia 50 ambao unaovikabili vituo vya Afya, Zahanati na baadhi ya Hospitali za Halmashauri na kuchangia kudhoofisha hali ya utoaji wa hudumaza Afya.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Julai 29, 2024 wakati wa Kongamano la kumbukizi la Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaa.

Amesema, mkutano huo utajadili masuala ya rasilimali watu kwenye Sekta ya Afya ambao ni uzalishaji wa wataalamu wa Afya ndani ya nchi, ubora wa watumishi wa Afya kwa kuhakikisha watumishi wanasalia kwenye maeneo waliyopangiwa kuhudumia wananchi.

Waziri Ummy amesema Hayati Rais Benjamini Mkapa alikua ni muumini na kinara waliofanya kazi kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za Afya ikiwemo Sheria ya Bima ya Afya ya NHIF aliyoiasisi Mwaka 2,000.

Kongamano hilo linakutanisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya ambapo watajadili masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya ambapo linatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Julai 30, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

AM/MTV News DRC