George Kivaya kiongozi wa shirika la raia katika eneo la Beni Mbau asema kusikitishwa na na mauaji ya watu inayo endelea wilayani Beni ambako vijiji na shamba za wakulima zaendelea kushambuliwa na kuwawa watu wasio kuwa na hatia.
Kivaya anasema vijiji vilivyo shambuliwa ni Mamove hasa Babila Bakaiko ambako sehemu kubwa wakaazi ni wakulima ambao hawana hatia yoyote .huku Isac Kinos kwa upande wake akiomba wabunge walio haidia wakaazi wa Beni usalama kurudi nyumbani kwa haraka kujadili kwa Pamoja swala la usalama na namna wakaazi waweza kulinda wenyewe.
Beni inashuhudia mauaji kwa muda mrefu Zaidi ya miaka kumi maelfu ya watu wakiendelea kufariki Dunia katika uangalizi wa Umoja wa Matifa MONUSCO ambao wana wanajeshi wengi DRC hasa Beni ambako kwa shuhudiwa mauaji lakini wakikaa kimia wakati wa mauaji hayo.
ADF hadi sasa haijawai kusema kwanini inawaua wakaazi kwa mapanga na visu.mauaji ya Mamove imekuwa na shaka kwani waliouwawa wengi wali uwawa kwa risasi na pikipiki zao kuchomwa moto ,japo ADF huua watu kwa mapanga na shoka na visu.