DRC

Watu wanao kuwa na silaha wadhidisha Mauaji ya watu katika mji wa Goma Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC.

Aprili 10, 2024
Border
news image

Kila siku mchana ama jioni kumekuwa kuMEripotiwa mauaji mjini Goma ,watu wakiuwawa na watu wenye silaha wanao shambulia watu ndani ya gari zao ama hata nyumbani kwao kwa saa za Mchana kama vile Jioni na usiku.Katika mwezi mmoja watu Zaidi ya kumi wakiwa wameuwa na watu wenye silaha barabarani kama vile nyumbani kwao.

Wakaazi wa Goma kwa sasa wakishindwa kuelewa kisa na mkasa wa mauaji ya sasa wakati ambao Mji wa Goma una wanajeshi wengi wa Umoja wa Mataifa yaani MONUSCO ,Kikosi cha SADC Pamoja na wanajeshi wengine kadhaa wanao husika na ulizni wa Mji wa Goma.

Kwa sasa kumekuwa sintofahamu kuhusu nani anae husika na ulinzi wa Mji wa Goma kutokana na wingi wa silaha na uwepo wa wanajeshi wengi Mjini .Vita mashariki mwa Congo ikiwa chanzo cha hali hii mbaya .wafanya biashara wakaazi wa kawaida wakiomba shuluhisho kwa mzozo wa DRC kwani sasa hali ya Maisha ni mbaya na ngumu isio eleweka.

AM/MTV DRC ONLINE