DRC/ BENI

WATU WA WILI WAUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KATA BENENGULE MJI WA BENI KIVU KASKAZINI.

FEBRUARI 14, 2024
Border
news image

Katembo ni mmoja wa wakaazi wa kata la Benengule kata moja ya Mji wa Beni ambayo yapatikana kusini mashariki mwa Mji wa Beni asema watu 2 wote wakiwa wanawake wame fariki Jumatano, Februari 14, 2024, katika mlipuko wa bomu pa Benengule Beu, Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). , kulingana na vyanzo vya ndani, Mbali na vifo hivyo, wengine wamejeruhiwa vikali. Kwa sasa, vyaonbo vya usalama vya serikali vimetumwa kwenye mahali pa tukio kwa uchunguzi zaidi kwani hadi sasa ni vigumu kufahamu mlipuko huo ume tokana Na Nini.

Beni na wilaya zake ni mmojawapo ya maeneo yasiyo na utulivu mashariki mwa DRC, ambayo yamekumbwa na ukosefu wa usalama kwa Zaidi ya miaka 10 kwa sasa watu wakiuwawa kwa mapanga visu ,shoka n ahata wengine kwa risasi kushambuliwa na watu wanao dhaniwa kutoka kundi la ADF

Beni imerekodi mfululizo wa mashambulizi yanayohusishwa na Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye mafungamano na wanajihadi wa Islamic State.matukio kama hayo yakiji wakati Beni kuna kikosi kikubwa cha Umoja wa Matifa MONUSCO ambao wako Beni na vifaa vingi vya kijeshi katika ulinzi wa raia lakini bado ulinzi huo ukiwa haupo . Wkaaazi eneo hilo wamekuwa MONUSCO kuondoka DRC kwani imesha shindwa kulinda raia ama hata kuhsindwa kuzuia mauaji ya Beni ambayo imesababisha wayatima ,wajane na vijiji vingi kubaki bila wakaazi vikichomwa Moto.

Germain Hassan KYAHWERE MTV-DRC ONLINE