DRC DJUGU WILAYA ITURI

ZAIDI YA WATU KUMI WA TEKWA NYARA NA SABA KUUWAWA NA KUNDI MOJA LA WANAMGAMBO ENEO LA DJUGU MKOANI ITURI

FEBRUARI 16, 2024
Border
news image

Utekeji nyara waendelea kushika kasi Mkoani Ituri ,wanao shutumiwa wakiwa watu wenye silaha kisa cha hivi karibuni kikiwa kile cha jioni juma tano katika maeneo matatu ya uchimbaji madini mukoani Djugu ndani ya Mkoa wa Ituri ambako wakaazi washutumu wanamgambo CODECO kuhusika ila wana mgambo hao bado kuthibitisha ,wakaazi wakisema watu wa CODECO Wali jitukiza eneo hizo wakirusha risasi angani kwa kwakuwatisha rai ana wachimba madini .

Taarifa kutoka mkoani Ituri wilayani Djugu ,zasema wapiganaji hao waliua wakaaji na kuteka nyara wengine walio bebeshwa mizigo na vitu walivio pora katika maeneo hayo. Walio asirika na vitendo hivio vya uzalimu ni wafanya biashara pamoja na wachimbaji wa madini eneo hilo la madini.

Duru zengine zasema kwamba, waasi hawa Wali tokeya ndani ya kijiji Njau na makofi Chabu na mahali pengine wakirusha risasi angani. Baada ya kuwasili ndani ya migodi, wanamgambo hawa waliwaua wakaaji saba mukiwemo wanawake tatu na mtoto mmoja, muchanga.

Jambo hilo, limelaumiwa na viongozi wa shirika la kirahia , wakishutumu ku ondoka kwa vikosi vya FRDC maeneo hayo bila ulinzi wowote na vikundi vya wanamgambo kuchukuwa mamlaka yaani uongozi wa vijiji. Kwa mjibu wa kiongozi eneo hilo, jeshi tiifu kwa serekali ya Drc limejipanga kwa ajili ya kukabiliana na wapiganaji ambao waendelea kuyumbisha usalama wa wananchi mkoani Ituri.

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS ONLINE