DRC HAUT KATANGA

WATU KUMI NA SITA WA FARIKI DUNIA NA ZAIDI KWA KIPINDU PINDU JIMBONI HAUT KATANGA.

JANUARI 31, 2024
Border
news image

Wakaaji wa Haut Katanga watolewa wito kwa kujikinga na ugonjwa wa kipindu pindu ambao umeripotiwa siku hizi jimboni humo. Duru hizo zimetibitishwa na waziri jimboni ahusikaye na afia.

Na kufwatana na kuzuka kwa Ugonjwa huo, waziri wa afia jimboni awataka wahimizaji, waandishi wa habari, viongozi wa ma zehebu mbali mbali, shirika za kirahiya pamoja na wataalamu wa maswala ya afia kwa ajili ya kuhimiza wakaaji kuhusu hatari ambayo inawatazama ju ya Ugonjwa huo.wakaaji hawa waombwa kuheshimu kanuni za afia kwa kujikinga kwa kutumiya maji Safi, ya kuchamuka pamoja na kujiosha mikono kila mara ili kujizuiza na hatari hiyo mbaya ambayo yasababisha vifo via walio wengi.

Eneo zile za afia ambazo Zina kumbwa na ugonjwa huo wa kipindu pindu ni kapempa, lubumbashi, kasanga, lukafu, kenya na eneo kadhaa jimboni humo. Imeripotiwa watu kumi na Sita kufariki dunia kwa Ugonjwa huo pamoja na sitini ambao waendeleya kuugua kwa Ugonjwa aripoti waziri wa afia akiomba wakaaji kunawa mikono na sabini kabla ya kula chakula, baada ya kutoka chooni, na kabla ya kunyonyesha na ikiwa mtu huendesha kidogo ama kuhara lazima ujielekeze kwenye kituo cha afia kwa ajili ya tiba ya zarura. Photo site le devoir

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online