DRC MAIKANGU

Watu thelathini wauwawa na ADF

JUNI 13, 2024
Border
news image

Watu Zaidi ya thelathini (30) wauwawa na watu wanao dhaniwa kuwa ADF katika Kijiji cha Maikangu katika secta ya Bapere wilayani Lubero Kivu Kaskazini,mauaji inayo sababisha wana vijiji kuhama na kukimbia vijiji vyao hadi katika Mji wa Njiapanda Mangurudjipa Kivu kaskazini mashariki mwa Congo DRC.

Kwa mjibu wa raia walio kubali kuongea na MTV nikwamba wakaazi kutoka vijiji vinavyo patikana katika eneo la Tukio wote wamehama vijiji vyao na kukimbilia katika mji wa Mangurudjipa na wengine kukimbilia Mji wa Butembo kutokana na usalama Mdogo.

Jeshi la serikali likiungana na wapiganaji wazalendo waripotiwa kuelekea eneo hizo kujaribu kukabiliana na ADF ambayo kwa sasa imekwenda kwa mwendo kasi kuwawa raia wasio kuwa na Hatia wilayani Beni na kwa sasa wakianza kuwawa watu wilayani Lubero ambako mkuu wa secta la Bapere ameomba serikali kuwalinda wakaazi dhidi ya mashambulizi.

Wiki moja sasa ADF imekuwa ikiwaua wakaazi katika Vijiji Tafauti wilayani Beni katika eneo la Kantine na kwa sasa wakivuka Muto Biena ambako waendelea na mauaji zaidi ya watu ,wengi wao wakiwa wanawake ,Watoto,vijana na watu wazima.

Wanao husika na mauaji wakitumia dini ya kiislmu wakati wa wakukata vichwa vya watu.

AM/MTV News DRC