DRC

Watu miambili wote wakiwa wakimbizi kutoka kambi mbali wazikwa katika usimamizi wa serikali mashariki mwa Congo DRC

SEPTEMBA 02, 2024
Border
news image

Akizungumuza mbele ya umati wa wananchi Gavana wa Kivu Kaskazini na wakaazi wa Mji wa Goma Meja Generali PETER Cirimwami aomba mataifa yote ya mbali kama vile ya karibu inayo chochea Mzozo mashariki mwa Congo DRC kuacha kwa maramoja kwani mauaji inayo fanyika DRC inatosha na inachosha sasa wakaazi .

Jeneza miambili (200) za watu mbali mbali yaani wazee,vijana,wanawake na vijana wanao fariki Dunia kutokana na vita mashariki mwa Congo iliwekwa mbele ya wakaazi ,ambao wengi wakiwa katika mshangao mkubwa ambao ni wa Uzuni na mshangao ,kuona jeneza miambili mbele za watu akisema mmoja wa wakaazi.

Vijana wa Lucha kwa upande wao wakishutumu serikali kushindwa kuhudumisha usalama wanainchi ndio sababu vifo vimeendelea kila siku swala ambalo wakimbizi wasema hawataendelea kuvumilia na watalazimika kurudi kwenye vijiji vyao iwapo hakuna suluhisho kwani sasa wamechoshwa na Maisha katika kambi

AM/MTV News DRC