DRC

Watu kumi na tatu walio zama maji tarehe tatu octoba katika ziwa Kivu wazikwa katika shamba la Mubimbi MINOVA Kivu kusini

OKTOBA 12, 2024
Border
news image

Baada ya ajali ya meli kufanyika katika ziwa Kivu karibu na Mji wa Goma tarehe tatu Octoba, serikali ikishirikiana na familia za watu walio fariki Dunia ,na mili yao kupatikana ,leo juma mosi imezikwa katika mji wa Minova Kivu Kusini daa ya sehemu nyingine kuzikwa alhamisi katika shamba la wafu la MAKOA wilayani Nyiragongo.

Familia zikishindwa kupokea tukio hilo ambalo ni ngumu na wengine bado wakiwa hawajapatikana baada ya meli hiyo kuzama maji.

Falilia zime miminika katika shamba la wafu la Mubimbi ambako wote wamezikwa kwa heshima

Hadi sasa idadi kamili ya watu walio fariki katika ziwaa Kivu kutokana na ajaliya meli haijulikane ila familia zikisema ni watu Zaidi ya miamoja ambao hadi sasa hawajapatikana.

Ikiwa wengine Zaidi ya hamsini na sita ndio walio ukolewa wakiwa hospitalini

AM/MTV News DRC