DRC

Watu 6 wauwawa na wapiganaji wenye silaha katika kambi ya wavuvi pa Musekere Mkoani Ituri Mashariki mwa DRC

AGOSTI 21, 2023
Border
news image

Mashirika ya kiraia Mkoani Ituri yatangaza kuuwawa kwa watu katika katika kambi ya wavuvi kandokando na ziwa Albert , umbali wa zaidi ya kilomita 100 kusini mashariki mwa Mji la Bunia mkoani Ituri . Miongoni mwa wahanga mtoto 1 , wana wake 2 na askari 2 , duru za kiusalama zime tuhumu wapiganaji wa kundi la Coodeco .

Kutokana na hali hiyo Familia nyingi zili lazimika kuhama makaazi yao , pia kuna watu 6 walio jeruhiwa kwa risasi . Innocent MADUKADALA ni Mkuu kiongozi wa sekta ya Banyali kilo wilayani Djugu anasema

"Ni wana mgambo wa Coodeco wana tenda mambo hayo karibu na ziwa Albert , wanajeshi pia wali shambuliwa na tena wavuvi nao tena waka shambuliwa . Hali haiya endeka vizuri na hivi ndiyo uliona ya kwamba wananchi walikuwa naomba ya kwamba waondoshe huu mda wa dharura , kusudi wana jeshi wafanye kazi waache kazi ya utawala "administration" tuna ongoja Raisi ikiwa kama ata amua nini kufatana na ombi ya Raia"

Licha ya mkataba wa usitishwaji vita mkowani Ituri , ulio sahiniwa na makundi ya wapiganaji sehemu hiyo ya kaskazini mashariki mwa Kongo , kundi la "Coodeco" lina kiuka mara kwa mara aina hiyo ya mikataba , ana sikitika Charité Banza kiongozi wa Kiraia Tarafani Bahema kaskazini

"Kukomesha mashambulizi ya Coodeco inafaa tu askari jeshi wafanye juhudi , na kilio yetu vilevile ni kuwapiga peke yake , watu wameisha uawa mingi sana kupora mali ya raia , iko lazima jeshi ifanye nguvu kupokonya siraha ili salama ikuwe ndani ya mji , aina yote ya mazungumzo ilisha fanyika mpaka sasa ile mazungumzo haija zaa matunda "

June 12, wapiganaji wa Coodeco wali wauwa wakimbizi 46 katika kambi hapo Lala kwa mjibu wa duru rasmi.

Eriksson LUHEMBWE/MTV