DRC-Goma

DRC WASIWASI KUHUSU HALI YA KIUTU KATIKA MJI WA GOMA

FEBRUARI 16, 2024
Border
news image

Baadhi ya kaaji wa MJI GOMA kIVU KASKAZINI kwa sasa, wapitia changamoto nyingi katika kupambana na hali ya kiutu mda huu wa vita vinavyo endelea Kati ya M23/RDF na jeshi la kongo FARDC pia kundi la vijana wazalendo.

Mama Treiphodi ni mkaazi wa Mji wa Sake alilazimishwa kukimbia Mji wake kutokana na mashambulizi ya waasi wa M23 ,kwa sasa apatikana katika Kata la Mugunga Magharibi mwa Mji wa Goma asema Hali ya kiutu imeonekana kua ngumu kwake Pamoja na wenzieikiwemo vile wakaaji wa Goma baada ya wakimbizi wa vita kuwa wengi Mjini Goma Kivu kaskazini mashariki mwa DRC.wengi wao wakitoka katika vijiji mbali mbali pembezoni mwa Goma ambako kwa shuhudiwa mapigano makali kati ya M23 na jeshi la serikali FARDC wanao twangana na waasi wa M23; jeshi ya kongo ikiungwa mkono na kundi za vijana wazalendo kalinda usalama wa mji SAKE,Masisi na wengine kutoka pande za NYIRAGONGO na RUTSURU.

Katika jiji la GOMA, imejulikana kwamba familia zinazo wapokea wakimbizi toka eneo za mapigano kua wana ugumu waku wa gharamia wakimbizi hao, hasa kuwalisha kulingana naku pandishwa kwa bei ya chakula na upungufu wa vipimo vya chakula.

Na Hali ya kuchumi ikididimia hii kutokana na kufungwa kwa barabara nyingi zinazo rahisisha usafiri wa vyakula kutoka mashambani kuelekea mji wa GOMA, wakielezea wafanya biashara wa chakula katika Soko tofauti Mjini Goma,wakaazi kama vile wakimbizi wa ndani wakitia matatizo mengi na kuhofia maisha yao. Pamoja na matatizo hayo dola za marekani zikipanda mnara na kuangusha Franga za Congo inayo ongeza ugumu wa Maisha Zaidi.

Mbali na ugumu waku wahudumia wakimbizi wa vita kimalisho, familia nyingi na wakaaji wa Goma,wameshindwa kulea baadhi ya familia zinazo pata uhamishono katika Nyumba mbali mbali kupata hifadhi ya muda ,wengine wakibaki katika Kambi mbali mbali ambako vile hawana Msaada wowote wa Chakula kama Vile dawa na huduma nyingine.

Nusrah Saanane