DRC ITURI

MA MIA YA VIJANA KUTOKA MAKUNDI YA WANAMGAMBO CODECO NA WA ZAIRE WAAMUA KUTO ENDELEZA UASI DHIDI YA WAKAAJI WILAYANI ITURI...

FEBRUARI 14, 2024
Border
news image

Makundi ya waasi wilayani Ituri imetangaza kusitisha mashambulizi dhidi ya raia .Hatua hiyo imechukuliwa katika kikao cha uhimizaji kuhusu amani mkoani Ituri hatua ilio fanikiwa kufatia hatua za viongozi wa serikali na kiasili katika lengo la kuhudumisha amani na usalama kati ya makabila mbali mbali mkoani Ituri ..

Mikutano kuhusu mchakato huo ilifanyika Mkoni Ituri eneo la bahema, Balendu chali na uhimizaji huo utaendelea katika maeneo mengine wakisema viongozi wa kiasili . Wanamgambo wanao shikilia silaha wamekuwa kwa mara kadhaa chanjo cha ukosefu wa usalama maeneo mengi wilayani Ituri hususani Djugu wakiendeshawakishutumiwa kuhusika katika mashambulizi na mauaji ya watu wasio kuwa na hatia , uporaji pamoja na wizi ya mali ya wakaaji .

Wote wakikubaliana sasa kujenga umoja kwa ajili ya amani na uaslama katika eneo zao .Ituri kwa Mda mrefu imeshudia machafuko,mauaji,uhalifu wa kivita inayo sababisha mkoa huo kutoendelea japo kuna madini mengi na mali ya misitu.mkoa wa Ituri unapakana na taifa la Uganda kupitia Ziwa albert na sehemu nyingine ikiwa karibu na Soudani Kusini.

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online