DRC SADEC /SAMIRDC

WANAJESHI WA WILI KUTOKA AFRICA WALIO UWAWA NA M23 WAREJESHWA NYUMBANI KWAO.

FEBRUARI 21, 2024
Border
news image

Nikupitia uwanja wa ndege wa Goma ,mili ya wanajeshi wa wili kutoka taifa la Africa walio uwawa kwa kuvurumishwa Bomu na M23 katika Mji wa Sake wamerudishwa nyumbani hii juma nne .hii imefanyika baada ya hutuba mbali mbali kufanyika kwenye makao makuu ya SADEC Mji Goma ,ambako kulifanyika sherehe za kuaga mili hiyo.

Akichukuwa kauli wakati wa hutuba mbali mbali ,Gavana wa Kivu Kaskazini Meja Generali Piter Cirimwami asema serikali ya Congo yapongeza juhudi ambazo kikosi cha SADEC yaani SAMIRDC imeonesha wakati wa Ushirikiano wake na jeshi tiifu kwa serikali.CIRIMWAMI amesema kuwawa kwa askari hao wa wali wa Africa kusini imeonesha tihio kubwa ambalo wanalo waasi wa M23 ambao wana saidiwa na taifa Jirani la Rwanda .Na hii iwe mwanzo wakusiimua wanajeshi wote kujihami kwakukabiliana na M23 ambao anasema tishio kwa usalama wa DRC na mmoja wapo wa watu wanao sababisha hali mbaya ya kiutu na Maisha ya wakaazi kuwa magumu.

Africa Kusini ni mmoja wapo wa mataifa ilio leta wanajeshi wake mashariki mwa Congo Pamoja na Tanzania baada ya ya kikosi cha Africa Mashariki kuondoka kwani kilishutumiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kupambana na kundi la waasi wa M23 .Africa Kusini inashirikiana na Tanzania ,Malawi katika makabiliano na uasi wa M23 katika Mji wa Sake wilayani Masisi kilometa Zaidi ya ishirini maagharibi mwa Mji wa Goma .

Wiki ilio pita mapigano makali yalizuka kati ya M23 na jeshi la serikali likiungwa mkono na wazalendo Pamoja na jeshi Rafiki la Burundi ,kwa bahati mbaya M23 ilivurumisha mzinga toka kwenye milima ya Mushaki na Malehe na kuanguka katika Kambi ya wanajeshi wa Africa Kusini ,ambako wanajeshi wa wili walifariki Dunia na wengine kujeruhiwa.

Hadi sasa SAMIRDC yaani SADEC haija sema lolote kuhusu mashambuli hayo .ila SADEC ikitoa tahdhari kwa taifa lolote litakalo nshambulia wanajeshi wake kuwa itakuwa ni uchokozi ambao hauta vumilika kushambulia mwana memba wa SADEC bila sababu yoyote.

AM /MTV DRC ONLINE