DRC GOMA

WANAHABARI KATIKA MJI WA GOMA KIVU KASAKAZINI WAPATA MAFUNZO KWA KUSHINIKIZA ULINZI WA MBUGA LA VIRUNGA KIVU KASKAZINI MASHARIKI MWA DRCONGO.

MACHI 18, 2024
Border
news image

Mwishoni mwa wiki waandishi wa habari zaidi ya ishirini walipata mafunzo namna ya kushinikiza ulinzi wa mazingira Kaskazini.waalimu walisisitiza kuhusu utaalamu katika uandishi Habari hasa kuandika uhakika na kuwa na ujuzi wa kutosha Pamoja na kutafuta Habari zilizo sahihi. Bienvenue Bwende kutoka ICNN alisema warsha hii haiku kuwa tu kubadilishana habari zinazohusiana na uhifadhi wa Mbuga la Wanyama porini lakini pia, kuinua hisia zinazopaswa kuzingatiwa wakati na toa taarifa ambazo zaweza kusukuma gurudumu za maendeleo hasa katika secta ya ulinzi wa Mazingira.

Bwende aomba wa pasha habari ku zingatia na ku pasha Taarifa nzuri na ya uhakika .na kujenga ushirikiano kati ya Virunga parc na jamii jirani", ambayo inahitaji usambazaji wa habari nzuri.hawa waomba wataalamu wa vyombo vya habari kuwa na nyaraka zote kuhusu masuala ya uhifadhi.

Kwa upande wake Tuver Wundi, mmoja wa wakufunzi aomba waandishi wa habari wawe na maelezo kwanza kabla ya kutangaza stori zao zinazo husu mazingira, ili kuielezea na kufahamisha vyema uma kuhusu ulinzi wa mazingira na umuhimu wake.

Methode Uhoze wa ICCN alisisitiza kuhusu PNVI na umuhimu wake katika uchumi na uimarishaji wa jimbo la Kivu Kaskazini akitoa mwito kwa makundi mbali mbali kuchangia katika uhifadhi bora Zaidi wa mazingira . washiriki, wanataka kuona mipango hii kuendelea kati ya Hifadhi ya Taifa ya Virunga na waandishi wa habari kitaaluma, ili waandishi wa habari wawe na maelewa ya kutosha tosha kwa ajili ya matangazo mazuri kuhusu mazingira.

Nadège Mulemba MTV.