DRC KIVU KASKAZINI

Wanafunzi 155,969 wa somo la kiprimari wanaotarajiwa wote kushiriki mtihani wa ENAFEP 2024 mkoni

JUNI 04, 2024
Border
news image

Mtihani wa Kitaifa wa Kumaliza Shule ya Msingi (ENAFEP) umeanza Jumatatu hii, Juni 3, 2024 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika jimbo la Kivu Kaskazini, licha ya hali ya usalama inayotia wasiwasi, wanafunzi walihudhuria mitihani wa shule ya msingi tangu jana kote.

Katika Mitihani hiyo haikupelekwa katika eneo zinazo dhibitiwa na waasi wa M23 ,ikiwa mpango wa serikali.Katika hafla ya kuanza kwa ENAFEP, Prisca Luanda Kamala, mshauri anayesimamia Elimu kwa gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, alikaribisha azimio la mamlaka ya kuendelea na masomo ya wanafunzi kama sababu ya amani Usalama na maendeleo licha ya vita vya uvaamizi dhidi ya DRC kutoka taifa la Rwanda.

Kwa jumla, watashiriki wanafunzi 155,969, wakiwemo wasichana 78,357 na wavulana 77,605, amabo wako katika vituo 552 vya mitihani, kukabiliwa na majaribio ya maandishi na ya mdomo ambayo yatafanyika kwa siku mbili.

"Pamoja na hali ya vita inayo tulazimisha Rwanda, mamlaka imechukua hatua zote kuhakikisha kuwa mitihani inafanyika kwa amani .Katika maeneo yanayo zibitiwa na M23, hususan Rutshuru, Masisi na Nyiragongo, vituo vya kufanyia mitihani vimehamishwa kwenye mji wa Goma, na kaina wilayani Lubero kuepuka mwaka tupu katika maeneo haya", alitangaza Prisca Luanda Kamala, mshauri ana simamia Elimu kwa gavana wa mkoa.

Utakumbuka kwamba , vituo vya mitihani vilivyoko katika miji ya Kanyabayonga na Bulotwa, katika eneo la Lubero, pia vimehamishwa hadi katika Mji mdogo wa Kayna. Uamuzi huu unafuatia vitisho kutoka kwa waasi wa M23-AFC wanao ungwa mkono na Rwanda DRC ikisema ,huku waasi wa M23 bado wakijaribu kuteka vijiji vinavyo zunguuka mji wa kanyabayongaWilayani Rutshuru, na kusababisha wimbi la watu kukimbia makazi yao wakihufia usalama wao.

Huku jeshi la serikali likiendelea kukabiliana na waasi hao katika eneo mbali mbali karibu na mji wa Kanyabayonga ambao sehemu mmoja ipo wilayani Lubero na sehemu nyingine ipo wilayani Rutshuru.

Daniel Bisongo - MTV DRC