DRC
Walinda amani wa JWTZ chini ya MONUSCO wanaohudumu nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametoa msaada kwa watoto yatima ambao wamepoteza wazazi wao kutokana na migogoro inayoendelea nchini humo.
NOVEMBA 07, 2024
Kamanda wa Kikosi cha 11 cha Tanzania, Luteni Kanali Verdasto Ernest Kikoti, ameongoza zoezi la utoaji msaada huo na amesema pamoja na jukumu la msingi walilonalo la ulinzi wa amani nchini DRC, wameguswa kuwasaidia watoto yatima kwa sababu yanapotokea machafuko, wanaoathirika ni watoto na wanawake. Kwa hivyo, wataendelea kuwasaidia kwa kuwapatia mahitaji muhimu kwa kadri watakavyoweza.
Aidha, Bi Masika Kombi Prisca, Kiongozi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mungu ni Mwema kilichopo Boikene mjini Beni, amewashukuru walinda amani wa JWTZ.
Walinda amani hao wametoa magodoro, sabuni, chakula, madaftari, kalamu, mafuta ya kula na vifaranga vya kuku.