DRC

Wakimbizi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo waomba serikali kuwarudisha kwenye vijiji vyao kuliko kubaki kambini katika mateso

JUNI 20, 2024
Border
news image

Ulimwengu Pascale mkimbizi kutoka Mji wa Sake wilayani Masisi amevunjika moyo kutokana na hali ya kimaisha anayo pitia Pamoja na Watoto wake na mimiea na Mifugo yake yote ikiwa imesha ibwa na watu wenye silaha baada yay eye kukimbia nyumba yake wakati wa mapigano kati ya M23 na jeshi la serikali FARDC.

Pascale anasema yeye na Watoto wake kwa sasa wanaishi vibaya katika hema moja ambako aendesha Maisha akiwa na Watoto wasichana na wavulana wote wakilala Pamoja wakiwa Watoto saba .Mzee huyu asema kwa sasa ameshindwa hata kulalamikia viongozi kwani sauti zao kwa sasa zimechoka kwakulalamikia upatikanaji wa amani.

Wakimbizi wamesema hayo leo ikiwa tarehe ishirini ambayo imewekwa kwa ajili ya wakimbizi ,DRCongo ikiwa na sehemu kubwa ya wakimbizi Kivu Kaskazini wengi wanao kimbia makaazi yao kutoka Rutshuru,Masisi,Nyiragongo ,Beni na Lubero kwa sasa ambako semeu mmoja ni mapigano ya M23 na jeshi la serikali na sehemu nyingine ADF.

Wote kwa jumla wakiomba amani na usalama ili warudi kwenye vijiji vyao kuliko kupewa misaada isio tosha kambini.

AM/MTV News DRC