DRC

Wakimbizi Kambi mbali mbali Mjini Goma na Nyiragongo Waomba Marekani Kushurutisha Rwanda Kuondoa Majeshi ili Warudi Nyumbani

JULAI 19, 2024
Border
news image

Wakimbizi wanao patikana katika kambi mbali mbali Mjini Goma na Nyiragongo waomba Marekani kushurutisha serikali ya Kigali yaani Rwanda kuondoa majeshi yake kwenye vijiji vyao ili warudi nyumbani kwao.

Masaa macache baada ya serikali ya Marekani kuongeza muda wa usitishwaji wa Mapigano mashariki mwa Congo DRC ,inayoendelea kati ya M23 na jeshi la serikali ya Congo FARDC wakaimbizi wanao ishi katika kambi mbali katika taifa hili wanasema kwamba wanacho kihitaji ni amani .

Ciza Samuel ni mmoja wa wakimbizi walio kimbia vijiji vyao ,kutokana na mapigano ilio kuwa ikiendelea kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 ,kwasasa amekuwa mlamavu akiwa kambini baada ya kupigwa risasi akiwa katika hema yake.Hali inayo wagusa akina mama kama mama huyu ambae tumekutana nae katika kambi hii ya kanyaruchinya .

Baadhi ya wakaazi na wachambuzi wa siasa wakishutumu Marekani na Ulaya kuunga mkono waasi wa M23 na serikali ya Rwanda kuyumbisha usalama mashariki mwa Congo ambako malefu ya watu wapitia hali mbaya na ngumu katika kambi mbali mbali.

AM/MTV News DRC