Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa amewasili leo Mjini Goma Kivu kaskazini mashariki mwa taifa lake akishinikizwa na mawaziri Zaidi ya Kumi Pamoja na wabunge na maseneta Suminwa anasema amekuja kutasmini hali halisi kuhusu uongozi wa kijeshi na kuwasikiliza wakaazi hasa mashirika ya kiraia. Uongozi wa kijeshi ukiwa umefanya miaka mitatu hadi sasa.
((Nimekuja kukutana na wakaazi Pamoja na mashrika ya kiraia na wananchi wenyewe watuambie nini wana kitaka kuhusu uongozi wa kijeshi kwani Rais alichukuwa hatua nyingi kuangalia namna na kupunguza hatua ya uongozi wa kijeshi ndio sababu nimekuja hapa kukutana na wananchi wenye))
Diane June Mukeshimana ni mbunge Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo kwa upande wake akisema hajaona umuhimu wa uongozi wa kijeshi kuendelea kwani hakuna hata eneo moja lilo chukuliwa na jeshi tangu uongozi wa kijeshi. Kambele Kiviri mbunge wa Lubero aomba waziri mkuu kutekeleza mahitaji ya raia kuondoa uongozi wa kijeshi Ituri na Kivu Kaskazini.
Waziri mkuu ametembelea mashariki mwa Congo bado hali ya usalama ikiwa tete Mjini Goma kutokana na mauaji kila siku na wakaazi walio kimbia vijiji vyao bado wakibaki makambini bila msaada na eneo nyingi zikiendelea kubaki mikoni mwa M23 swala linalo wakera wakaazi Pamoja na wabunge. Asijari nyalamba ni kingozi wa UDPS cha tawala Kivu Kaskazini kwa upande wake asema ni muhimu kuondoa Uongozi wa kijeshi kwani uongozi wa raia kwa mtihani mkubwa unao kuja kubalisha katiba.
Baada ya Mkoa wa Kivu Kaskazini suminwa nakwenda Bunia Mkoani Ituri ambako vilevile wakaazi wamelalamikia hali ya uongozi wa kijeshi. Mumbere Bwana pua mbunge wa Goma akiwa katika msafara wa Waziri mkuu..
Leo jioni hii Waziri akianza kuwasikiliza wakaazi kupitia tabaka mbali mbali.