DRC

Wakaazi wa Mji wa kanyabayonga wilayani Lubero walalamikia hali mbaya na ngumu ya usalama eneo lao inayo sababishwa na uasi wa M23

JUNI 06, 2024
Border
news image

Baada ya kukimbia vijiji vyao na kuwa wakimbizi katika mji wa Kanyabayonga na baadae kukimbilia katika Mji wa Kirumba waakaazi kutoka vijiji. Inavyo shambuliwa na kutekwa na waasi wa M23 waomba serikali kupitia jeshi la serikali ya Congo kulinda usalama wa wananchi wilayani Lubero ambako mabomu imeanza kuwashambulia watu wakiwa Nyumbani kwao.

Leo hii bomu Zaidi ya Tano zilianguka katika Mji wa Kanyabayonga wilayani Lubero na kuharibu makaazi ya watu .vijana wanao baki katika mji huo Pamoja na wanawake wakiomba Umoja wa Matifa MONUSCO kuhakikisha usalama wananchi unalindwa kwani wengi kwa sasa wako hatarini kutokana na mabomu kushambulia makaazi ya watu.

Akiwa ziarani Lubero Mumbere Bwana Pua mbunge wa Goma aomba ushirikiano wa wananchi .wazalendo na wanajeshi katika harakati za kupambana na waasi wa M23 .Pua amesema Hospitali nyingi kwa sasa hazina Tiba wilayani Lubero na Kirumba ,kinacho hitajika ni kuomba wafadhili na serikali kupeleka madawa kwa haraka katika vituo vya afia ambavyo vimefurika wagonjwa.

Hali ikiendelea kuwa ya wasiwasi mapigano bado yaendelea kwenye milima inayo patikana karibu na Mji wa Kanyabayonga .waasi wa M23 wakiwa wamerudishwa nyuma.

AM/MTV DRC ONLINE