DRCongo BENI /MAIVIVI

WAKAAZI WA MJI WA MAVIVI WILAYAN I BENI KIVU KASKAZINI WAOMBA SERIKALI KUIMARISHA USALAMA ZAIDI.

JANUARI 25, 2024
Border
news image

Siku moja baada ya watu wenye silaha kushambulia wakaazi katika Mji mdogo wa MAVIVI wilayani Beni ,wana vijiji vya Ngite na Mji wote wa MAVIVI waomba serikali hasa Rais wa Congo Felix Tshisekedi kutafuta suluhisho la haraka kuhusu usalama wa wananchi kwenye vijiji vyote vya Beni.walio nusurika mauaji hayo wakisema watu wenye silaha na mapanga walionekana kwenye mashamba nyakati za jioni ,pembezoni mwa Mavivi lakini vyombo vya usalama vilianza puuza taarifa zao ndio sababu watu waliuwawa .

Mmoja wa viongozi wa mahali asema ni mshanago mkubwa lkuona vyombo vya usalama vilipewa taarifa lakini hawakutenea kazi taarifa hizo ndio sababu maafa yalikuwa mengi Zaidi ,Bwanakawa anasema watu tanu wote waliuwawa kwa risasi na wengine kwa mapanga kwa saa za usiku na mtoto mmoja alitekwa hadi sasa haijulikane wapi alipo .

Mamama mmoja alie hifadhi jina lake asema kwa sasa wamechoka na hali ya ukimbizi ,vilio na kuhangaika kila siku wakati kuna jeshi na viongozi wanao chaguliwa ambao huhaidia usalama wakaazi.Mama huyu ameomba Rais kufanya jitihada zote kuhakikisha usalama wa watu na vitu vyao unapatika,na wengine wakidhani kuwa muhimu nikuweka vijana wazando katika kila kijiji kwakuweza punguza mashambulizi ya watu wanao dhaniwa kuwa ADF.

Mavivi ina kambi kubwa ya kikosi cha Umoja wa Mataifa MONUSCO na jeshi la Congo FARDC lakini bado ADF ilifanikiwa kutekeleza shambulio.eneo hilo lilikuwa tayari limepata usalama kwa Zaidi ya miaka mitano bila kushuhudia mauaji.

AM/MTVĀ ONLINE.