DRC

Waislamu mashariki mwa Congo wameungana na ulimwengu kusherekea sikuku kubwa ya Aïd-el-Fitr katika mazingira ya ukosefu wa amani na Usalama.

Aprili 10, 2024
Border
news image

Mustafa Kemal Mulopwe muislam Mjini Goma asema siku ya Eid-el-Fitri nchi DRC hasa Kivu Kaskazini imekuwa tafauti na nyingine Kote Duniani , kutokana na wasiwasi kubwa ,polisi na vyombo vya usalama vikiwekwa kote Mjini Goma baada mea wa Mji kupiga marufuku mikusanyiko ya waislamu katika viwanja vya uma kutokana na hali ya kiusalama. Mulopwe nasema kiongozi wa waislamu Mjini Goma alitoa maelekezo kuhusu mwenendo ambao waislamu waweza kuzingatia kutokana na hali ya kiusalama kwa sasa.

Siku ammbayo Wengine wapitisha EID-El Fitri wakiwa katika kambi za wakimbizi wa ndani kutokana na vita vya M23 ambao wapitia hali ngumu na mbaya ya kimaisha . Sabiti Djaffar Al Katanty amekuwa musatari wa mbele nakushuhudia mateso wanayo pitia waislamu kambini kama anavyo sema Sabiti Djaffar Al Katanty Djaffar ameomba Taifa la Rwanda na wengine kuondoa wanajeshi wake nchini DRC ili waislamu na wasio waislam warudi vijiji kwao kuendelea na milimo pamoja na shughuli nyingine za kimaisha.

Waislamu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiomba watu wote wanao changia katika machafuko mashariki mwa Congo kuwa na moyo wa huruma kwani mwanadamu haitwi kumtesa mwenzake ama kumwanga Damu ,inayo hitajika ni kila mmoja kuchangia amani na usalama Pamoja na umoja.

AM/MTV DRC ONLINE