DRC
Wafungwa Mia Moja Kumi Na Saba Waachiliwa Baada Ya Kusamehewa Na Rais Wa Congo DRC. Miongoni Mwao Wanawake Na Wanaume
APRILI 8, 2025
Wafungwa miamoja kumi na saba waachiliwa baada ya kusamehewa na Rais wa Congo DRC. Miongoni mwao wanawake na wanaume.
Jaji wa Mahakama ya Kiraia na Kijeshi wa Beni mnamo tarehe 8 Aprili 2025, Mwendesha Mashtaka wa Umma MANGA WENYE Junior na mkaguzi wa gereza la HUBERT wa Beni wametumia sheria ya kuachiliwa kwa msamaha wa rais na kupunguzwa kwa kifungo katika Gereza la Kangbayi.
Huku wengi wakiwa na makosa tafauti, baadhi ya wafungwa miamoja kumi na saba (117) wa kike na wa kiume wameachiliwa huru nae Gavana wa Kivu Kaskazini SOMO. KAKULE Evariste, ambaye alikabidhi nyaraka za msaada kwa walengwa wa kutolewa kwa siku hiyo.
Somo ameomba wafungwa wa kijesho wote kuelekea katika kambi ya mafunzo ya Nyaleke moja kwa moja.