TANZANIA

WAFANYAKAZI WAZEMBE MSIMFANYE DK. SAMIA KUOMBA KURA KWA KUPIGA MAGOTI

FEBRUARI 05, 2024
Border
news image

Katibu wa NEC Itikadi , Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda akiwa mkoani Katavi amewakanya viongozi wazembe waliopata bahati ya kuongoza kuhakikisha wanawasikiliza na kutatua changamoto za wananchi wanyonge na ndio dhamira ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, na kama mtu akijisahau kutekeleza wajibu wake basi hata Mungu anakuondoa na kuwapa nafasi watu wengine.

"Mwenezi mimi Makonda nimehapa hata watumishi wazembe sina huruma nanyi, hatutaki kumuona Mwenyekiti wetu na Rais Dkt. Samia anakuja kuomba kura kwa kupiga magoti kisa uzembe wako wewe Kiongozi, Mtendaji au Mtumishi wa Serikali...mkifanya kazi zenu vizuri bila malalamiko basi haki itatawala na wananchi watakua na furaha na nchi yao".

"Chama chochote cha Siasa kikiacha kushughulikia kero za Wananchi kitapoteza haki ya utawala na tumekubaliana tabia ya Wabunge kusubiria kipindi cha uchaguzi ndio kuanza kutoa pesa ili wapendwe hatutaki na msemaji wa CCM ni mimi Makonda , nitasema kwa maoni ya Wananchi kwanza cheo badae".

MTV Tanzania