TANZANIA

Wadau Sekta ya Afya Wakabidhi Vitendea Kazi vya Thamani ya Milioni 800 kwa Serikali

FEBRUARI 24, 2024
Border
news image

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea vitendea kazi vyenye thamani ya Milioni 800 kutoka kwa wadau wa CDC kupitia THPS kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI na Kifua Kikuu katika Mkoa wa Tanga Nchini Tanzania.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amepokea vitendea kazi hivyo leo Februari 23, 2024 Mkoani Tanga ambavyo ni pikipiki 50, friji 72, Centrifuges 56, Compyuta 50, UPS 50 na printa 50 ambavyo vitendea kazi hivyo vitaimarisha huduma za Afya katika Mkoa huo.

Wakati akipokea vitendea kazi hivyo Waziri Ummy amewataka wote watakaokabidhiwa vifaa hivyo kuvitumia Kama ilivyo elekezwa ikiwa ni pamoja na kuwafikia wateja wanaoishi katika mazingira magumu na mbali na vituo vya kutolea huduma za Afya ili kuwafikishia huduma.

“Lakini pia tunaamini kwamba mtaongeza idadi ya huduma mkoba ‘outreach services’, kuwafikia wateja walio katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa ugonjwa wa UKIMWI na kuwapatia huduma za kinga zikiwemo

MTV Tanzania