DRC VICHUMBI

WAASI WA M23 WACHUKUWA MJI WA VICHUMI UNAO PATIKANA PEMBENI YA ZIWA EDWARD WILAYANI KIVU KASKAZNI.

MACHI 11, 2024
Border
news image

Mufula ni kiongozi wa vijana kutoka mji wa Kibirizi asema kwa sasa anasikitishwa na kuona Mji wa Vichumbi kuchukuliwa na waasi wa M23 mchana wa leo juma tatu mach 11 2024, Mufula amasema alikimbia mji wake akitembea kilometa ndefu kwa mguu lakini kinacho mshangaza nikuona jeshi la Congo kwasasa limerudi nyuma bila kupambana na waasi wa M23 ambao kwa sasa wamedhibiiiti mji Muhimu kwa usalama ziwani Edward.

Wakaazi wengi walio baki Mjini baada ya kujifungia katika nyumba zao walionekana wakihudhuria mkutano wa hadharani ulio itishwa na M23 ,ambao walionekana wakiomba wakaazi walio kimbia Mji wao kurudi nyumbani kwao ,M23 imetangaza kiongozi mpya wa VICHUMBI baada ya kiongozi mwakilishi wa serikali kumenya mbio kutokana na uasi wa M23.

Mapigano ilio pelekea wakaazi wengi kukimbia kwakutumia boti za maji wakikimbilia kwenye vijiji vyao vinavyo patikana kwenye milima mirefu inayo patikana pembezoni mwa ziwa hilo. Ziwa EADWARD lapatikana sehemu moja wilayani Rutshuru ,sehemu nyingine Lubero na sehemunnyingine wilaya ya Beni sehemu yake ya kaskazini Pamoja na upande wa mashariki ukiwa upande wa Taia la uGANDA na kusini ikiwa ni mbuga la Virunga.

Kuchukuliwa kwa Mji huo ni pigo kubwa kwa mbinu za kijeshi za serikali kwani hii ni eneo muhimu sana ki usalama.

AM/MTV DRC ONLINE