DRC

Waasi wa M23 wachukuwa Mji muhimu wa walikale Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC baada ya jeshi tiifu kwaa serikali FARDC na wapiganaji wazalendo kutimuka

MACHI 20, 2025
Border
news image

Katika pica walizo chukuwa katika kati mwaa Mji wa walikale mji mkuu wa wiliya hiyo muhimu kiuchumi kwaa uzalishaji wa madini, waasi wa M23 wameonekana na silaha na wengine na radio za mkono na hata wengine wakishangiliwa na wakaazi wa Mji huo.

Walikale ni mji mkuu wa wilaya ya walikale inayo patikana magharibi mwa Mji wa Goma ikiwa miongoni mwa wilaya nyingine nyingi ambazo zinaunga mkoa wa Kivu Kaskazini, hii ni wilaya ya nne kuchukuliwa na waasi wa AFC/M23 baada ya miji ya Goma Kivu Kaskazini na Bukavu Kivu Kusini. Jumhia ya kimataifa imekuwa ikiomba AFC/M23 kusitisha mapigano bila mafanikio.

Wiki hii M23 ili goma kwenda Luanda kushiriki mazungumuzo ilio andaliwa na msuluhishi wa Mzozo Rais wa Angalo kutokana na kile walichosema, kuwa kuna mataifa isio penda amani na usalama kupatikana DRC kwakuwawekea vikwazo viongozi wa M23.

Wakaazi wa Mji wa walikale hadi sasa washuhudia mlio wa risasi pembezoni mwa Mji wa walikale ambao una zunguukwa na misitu. Kuchukuliwa kwa walikale ni pigo kubwa kwani mkoa huo unaunganisha Mkoa wa Tshopo yaani Kisangani na mkoa wa Maniema, hii ikiongeza hofu Zaidi.

AM/MTV News DRC