Muungano wa Mto Kongo (AFC/M23) ulitangaza, Jumatatu Machi 17, ushiriki wake katika mazungumzo ya Luanda yaliyopangwa kufanyika Machi 18 chini ya mwamvuli wa Angola.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumatatu jioni, vuguvugu la waasi linashutumu vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya kwa viongozi wake kadhaa, wakiamini kwamba vinafanya mazungumzo kutowezekana.
"Vikwazo vilivyofuatana vilivyowekwa kwa wanachama wetu, ikiwa ni pamoja na vile vilivyopitishwa katika mkesha wa majadiliano huko Luanda, vinaathiri sana mazungumzo ya moja kwa moja na kuzuia maendeleo yoyote ili amani na usalama ipatikane mashariki mwa Congo DRC pamoja na kujenga umoja wa watu wa Congo DRC."
Jumatatu hii, Umoja wa Ulaya ulitangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa kundi hili lenye silaha linalofanya kazi mashariki mwa DRC na kuungwa mkono na jeshi la Rwanda kwa mji wa Umoja wa mataifa na Marekani pamoja na Ulaya.
Bertrand Bisimwa, mkuu wa mrengo wa kisiasa wa M23, Jean Bahati Musanga, "gavana" wa Kivu Kaskazini aliyeteuliwa na waasi, au hata Désiré Rukomera, anayehusika na uandikishaji na propaganda za M23, nae Jean-Bosco Nzabonimpa, naibu mkuu wa fedha wa kundi la waasi, wameathiriwa hasa na hatua hizi za Umoja wa nchii za Ulaya.
Vikwazo hivyohivyo vya Umoja wa Ulaya vinawalenga maafisa kadhaa wa Rwanda wanaoratibu operesheni za kijeshi mashariki mwa DRC, kuwaunga mkono waasi wa M23, pamoja na Francis Kamanzi, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Madini, na Gesi ya Rwanda (RMB), kwa jukumu lake katika usafirishaji haramu wa madini ya Kongo.
Ujumbe wa serikali ya Congo ukiwa tayari nchini Luanda Angola ambako yalitarajiwa kuanza leo hii kumi na nane.
Wakaazi mashariki mwa Congo wakionekana kuvunjika moyo kwani wengi hasa wanao ishi eneo la mapigano wakiomba kukomesha kwa vita kwa haraka kwani sasa wamechoka na hali ya ukimbizi wa mara kwa mara.
Huku mapigani yakiendelea wilayani walikale.