Kiongozi wa AFC/M23 Cornaille Nanga afungua Rasmi Benki Mpya kwa ajili ya kundi lao la waasi mashariki mwa Congo DRC, Nanga alifanya hivyo mbele ya wakaazi wa Goma, wanasiasa na wanajeshi wa M23 na mbele ya vyombo vya Habari.
Akizungumuza na wakaazi wa Mji wa Goma na wafuasi wa chama cha AFC/M23 Nanga amasema, wamechukuwa hatua ya kuanzisha Benki ya CADECO kutokana na hatua ya serikali ya Kinshasa kufunga Benki zote Mjini Goma nae neo zote zinazo dhibitiwa na waasi, hii ni baada ya vita vilivyo pelekea serikali ya Kinshasa kushindwa na kuacha mji wa Goma mikoni mwa waasi hao, hii nikujibu kwa mahitaji ya wakaazi Pamoja na kusaidia kupokea pesa za Kodi.
Nanga amesisitiza kwamba CADECO itakuwa Benki kama vile benki nyingine ambazo leongo lake nikusaidia wakaazi wa Goma na sehemu zito zinazo kuwa chini ya uongozi wa AFC/M23. Utafahamu kwamba wakaazi wengi kwa sasa wapitia maisha magumu kutokana pesa zao kuzuiliwa katika benki ambazo zote zimesha funga miliango yake kutokana na hali ya kiusalama.
CADECO ilikuwa ni Benki ya mkopo kwa wakaazi wa DRC lakini kwa sasa AFC/M23 ikitangaza kuwa ni Benki ambayo itajibu mahitaji ya raia wanao ishi katika eneo ambazo kwa sasa zimedhibitiwa na waasi hao, wataalam wasema ni Vigumu kwa CADECO kuwa benki kutokana na sheria za kimataifa. Huku wakuu wa CADECO mjini Kinshasa wakisema hawatambui hatua ambayo imechukuliwa na waasi wa M23.