DRC-Beni

WAASI WA ADF,WATISHIA KU SHAMBULIA MAKANISA MJINI BENI KWA MAKESHA YA PASAKA ASEMA MSEMAJI WA JESHI ENEO LA BENI.

MACHI 28, 2024
Border
news image

Akizungumuza Na vyombo vya habari Kapteni ANTONY MWALUSHAYI atangaza kwamba mji wa Beni Kwa sasa una wasiwasi kutokana na tishio la kushambuliwa na wapiganaji kutoka Kundi la ADF ambao wanaua na kuwateka wananchi katika maeneo mbalimbali hasa katika kata la Sayo Na matembo manispaa MULEKERA ambapo takriban raia ishirini wame uwawa tangu wiki ilio pita.

Wakiangamia katika mashambulizi tafauti , jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC likismea lipo makini Kukabiliana na vitisho vya shambulizi lolote la watu wenye silaha wakati huu ambapo wananchi wajipanga kusherekea Siku kuu ya pasaka. Jeshi laomba ushirikiano wa wananchi na vyaombo vya usalama kwa kuzuia mashambulizi inayolenga makanisa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.

Msemaji wa jeshi katika Mji wa Beni wa operesheni za kijeshi SOKOLA 1 Kapteni ANTONY MWALUSHAYI, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mjini Siku zilizo pita masaha chache baada ya mauaji ya raia Katika Kijiji cha sayo mjini BENI KIVU KASKAZINI. Hata hivyo, Anthony Mwalushayi ahakikishia Raia wa Beni Na kando kando kwamba hatua muhimu dhindi ya usalama wao zimechukuliwa na jeshi la Congo na lile la ulinzi la wananchi ya UGANDA UPDF kuzuia kila Jaribio yeyote yashambulio ya magaidi hawa wa ADF.

GERMAIN HASSAN KYAHWERE,MtvĀ online.