DRC VITA MUTAANI MASISI

MA ELFU ZA WAKAAJI WA SAKE NA PEMPEZONI MWAKE WA YA KIMBIYA MAKAAZI YAO KUTOKANA N'A MAPIGANO MAKALI

FEBRUARI 08, 2024
Border
news image

Wakaaji hawa wa muji huo wa sake na pempezoni mwake, wame ya kimbiya makaazi yao kufwatana na miliyo ya risasi pamoja na makombora zilizo sikika mapema leo hii kunako kilometa chache na muji huo wa sake.

Duru tunazo kutoka eneo hilo zasema kwamba, waasi wa M23 wakishirikiyana na RDF waliingiliya kati kambi ya kikosi cha Frdc pamoja na wazalendu na kuanja rushiyana risasi eneo la ndendero, malehe si mbali na muji wa sake. Hali hiyo ili wasukuma wakaaji kuya kimbiya maskani yao. Wengi wa wakaaji hawa, wame kimbiliya mjini Goma ni kata Mugunga ndilo laendelea kumpokeya Wakimbizi. Na huko, wakaaji wa Jawa na wasiwasi kufwatana na bumu ambazo za endeleya ku anguka eneo hilo la kata, nyuma ya mchana wa leo bumu lingine limeanguka mahali paitwapo kwa Jina maarufu amour . Mpaka jioni hi Wakimbizi waendeleya kuwasili ju mjini Goma wakihofiya maisha jeshi la serikali FARDC lasema limewarudisha nyuma waasi na kuwapa pigo kubwa n'a kwasasa Mji wa Sake ulieko kilometa zaidi ya ishirini magharibi mwa Mji wa Goma unalindwa vizuri na Jeshi la Serikali .bado wasi wasi ikiendelea

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online