DRC ITURI

Viongozi wa makundi yenye silaha Mkoani Ituri wondoka katika mji wa Bunia kuelekea Kinshasa mji mkuu wa Congo DRC.

Aprili 09, 2024
Border
news image

Makundi yenye silaha waliondoka Mji wa Beni juma pili kuelekea Mji wa Kinshasa aambako watakutana na wakuu viongozi kutokana na ukosefu wa usalama wa mara kwa mara mkoani humo. Hii ni baada ya kupokea aliko kutoka kwa mamlaka ya kitaifa lengo ikiwa ni kuwashirikisha katika taratibu za kutafuta amani na usalama mkoani Ituri lakini pia kuzuia hatua zozote za muungano za waasi hao kujiunga na uasi wa M23 wa Alliance fleuve Kongo wa Corneille Nanga.

Makundi ikiwemo codeco ,waasi la Zaire, Mapi, FRPI, FPIC na wengi wanao patikana mkoni Ituri ambako wamekuwa wakipambana kila siku kukicha na kusababisha wakaazi kuhama mkaazi yao.hatua ambayo imepongezwa na wakazi wa jiji la Bunia ambalo wakati huu lahiyaji kupata amani ya kudumu na kufanya miradi ya maendeleo.

Wengine wanasema hawaelewi jinsi serikali inavyo bembeleza vikundi vilivyojihami vinavyo husika na mauaji ya watu mkoni Ituri , kupora na kuchoma nyumba za watu.

AM/MTV DRC ONLINE