Kama viongozi hawafanyi kazi wasitegemee serikali itawabeba kwa wananchi au watatumia vitu au pesa kuwapa wananchi ili wawachague kwenye chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini Tanzania kwakua serikali imeshaamua kila mtu abebe haki yake kulingana na kazi zake na sio kubebebana mizigo.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa nchini Tanzania Paul Makonda wakati akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa eneo la Tegeta Dar es salaam ambapo amesema anashangaa kuona baadhi ya viongozi hawafanyi kazi wanasubiri kipindi cha uchaguzi wagawe vitu ili kuoewa kura.
"Niwaambie ndugu zangu chama kinafwatilia utendaji kazi wa viongozi walioko chini yake hii ikiwajumuisha wabunge, madiwani na wenyeviti wa mtaa na watapimwa kuona namna wanavyowasaidia wananchi katika kutatua kero zao kama kilivyoahidi kwenye ilani yake kwamba kitatatua changamoto za wananchi kwa kuwapa huduma bora na kuwafikia popote walipo bila ubaguzi",alisema Makonda.
Niwashauri wananchi msidanganyike kwa zawadi ndogondogo ambazo zitawqgharimu maisha yenu badae bali na nyie muisaidie serikali kusimamia na kuoata maendeleo kwa kushiriki kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo.