DRC/BENI

VIJANA WAOMBWA KUACHANA NA UTUMIAJI WA POMBE KALI BASHU WILAYANI BENI.

Aprili 16, 2024
Border
news image

Saddam Patanguli Kiongozi wa Bvijiji vya Bashu asema kwa sasa hali ya afia kwa vijana eneo lake ni mbaya kutokana na utumiaji wa pombe kali ambayo imekuwa hatarishi kwa Maisha ya wakaazi wa eneo lake .Patanguli aomba serikali kuwatafutia ajira vijiana kama njia moja ya kukomesha hali ya vijana kujikita katika utumiaji wa Pombe kali kwani siku za usoni itakuwa vigumu kuwapata vijana wenye nguvu ambao waweza tumikia taifa.

Saddam anasema eneo la Bashu kwa sasa lina shuhudia viwanda vingi vya kutengeneza mvinyo mbaya kwa afia ya wananchi mvinyo ambao ni shida kwa afaia ya wananchi wake hasa Vijana.Patanguli alisema iwapo hakuna ahatua itakayo chukuliwa na serikali kufunga baadhi ya viwanda vya pombe hakuna ujio bora kwa vijana kwani nyingi huharibu afia kwa vijana.

Namnukuu “Mtu mwenye umri wa miaka ishirini (20) kwa sasa ukimuona unadhani ana miaka arbaini (40) hii nimshangao kwa kizazi chetu kwa sasa,hatujui hii tabia imetoka wapi ,na serikali inatazama kimia ,sasa hatujui wote hawa wakiwa hivyo nani ataongoza serikali ama nani ataadibisha watu.

Vijana wengi wakisema ikiwa wanatumia pombe kali kwanza ni kukosa ajira,pili wamepoteza ndugu jamaa na marafiki katika vita,tatu ukosefu wa usalama unasababisha watu kunywa pombe ili mabandia wakija wamkute amalewa kuliko kuuwawa akiona macho asema kijana mmoja alie hifadhi jina lake.

Wengine wakitambua tataizo hilo kuwa ni mbaya kwa afia na serikali lazima kuweka sheria ya kuunda viwanda vya mvinyo na pombe kali lah sivyo katika miaka kumi Beni ,Butembo na lubero haina ujio kwa vijana timamu.

Nadege Mulemba