TANZANIA

Vijana Kutoka Mashirika Mbali Mbali Waandamana Kuomba Amani Kivu Kaskazini

MACHI 04, 2024
Border
news image

Wakiwa na mabango na bendera ya Congo DRC vijana wa Lucha na Filimbi wakiandamana na wengine katika Mji wa Goma mji mkuu wa kivu kaskazini wamekabiliana na polisi na wengine nane miongoni mwao kukamatwa na kuachiliwa baadae .

Vijana hao wanasema wameandamana kufatia kile wanacho kiita unyanyashwaji wa wananchi wakati huu ambao wakaazi wapitia hali ngumu na mbaya ya kivita.

Muhindo Mathale mmoja wa waandamanaji aomba serikali kutangaza rasmi kuwa Kivu Kaskzini ni mmoa unao kuwa katika Vita na kodi zote lazima kupunguzwa hasa kodi kuhusu chakula.

Waandamanaji hao walikekea hadi kunako ofisi ya Gavana ambako walisoma ujumbe walio elekeza moja kwa moja kwa rais wa taifa wakiomba Rais mwenyewe kuchukuwa hatua kubwa kuhusu vita mashariki mwa Congo ambako wakaazi wamelazimika kuhama makaazi yao kwa sasa wakiwa bila chakula n ahata wakishuhudia ukosefu wa tiba.

Mshahuri wa Gavana Generali DANY YAMGBA amepokea malalamiko ya waandamanaji na kuwaonya kuwfanya sheria hasa kuepuka kunadamana kila mara kwani adui wa Taifa aweza tumia maandamano yao kuharibu usalama wa Mji wa Goma.

AM/MTV DRC ONLINE